Marko 1:2 inasema, “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako.” Ndugu zangu waamini, unaweza kuipata haki ya Mungu ikiwa tu utatupilia mbali uelewa wa kale na kuifuata Biblia kadri Neno la Mungu linavyokuongoza. Hivyo, wakati unaposoma Neno la Mungu, ni lazima ulisome hali ukiwa umeyaacha mawazo na tamaa zako za mwili. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo unapoweza kutambua na kuamini katika mapenzi ya Mungu ambayo anataka kuyatimiza. Kanuni hiyo inatumika pia katika kifungu cha Maandiko cha leo. Ni pale tu utakapokuwa umeyaachilia mbali mawazo yako ya kimwili na kisha ukalifuata Neno la Mungu linapokuongoza ndipo unapoweza kufahamu kiusahihi huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu.
https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35
Watu wengi hawafahamu ni kwa nini Yesu alikuja hapa ulimwenguni na akaupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji. Lakini ni lazima tufahamu vizuri kuhusu dhumuni...
Hata Wakristo wa leo wanakiri kuwa wanamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wao, lakini wengi wao hawafahamu kuwa Yesu ni Bwana aliyetukomboa toka katika dhambi...
Yohana Mbatizaji alikuwa akiuhuburi nyikani ubatizo wa toba wa ondoleo la dhambi. Si hilo tu, alikuwa ni mtu ambaye ataufanya ubatizo wa Yesu ambao...