Uhusiano Kati ya Huduma Ya YESU na Ile Ya YOHANA MBATIZAJI Kama Ilivyoandikwa Katika Injili Nne

Agano Jipya linaanza na Injili Nne ambazo ni Mathayo, Marko, Luka, na Yohana. Injili zote Nne zilishughulika na ziliandika kikamilifu kuhusu huduma ya Yohana Mbatizaji. Hii ni kwa sababu huduma yake ni ya muhimu sana. ...more

About the Show

Agano Jipya linaanza na Injili Nne ambazo ni Mathayo, Marko, Luka, na Yohana. Injili zote Nne zilishughulika na ziliandika kikamilifu kuhusu huduma ya Yohana Mbatizaji. Hii ni kwa sababu huduma yake ni ya muhimu sana. Hatuwezi kudai kuwa tunaifahamu huduma ya Yesu Kristo pasipo uelewa wa huduma ya Yohana Mbatizaji. Kama ndivyo, basi tunaweza kujiuliza, "Je, huduma ya Yohana Mbatizaji iliandikwa katika Injili Nne kwa umuhimu kiasi hicho?" Hali akimzungumzia Yohana Mbatizaji, Yesu alisema, "Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja" (Mathayo 11:14). Hivyo, Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtu aliyezaliwa katika dunia hii ili kuitekeleza huduma maalumu. Pia Yesu alisema, "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka" (Mathayo 11:12). Hii ni kweli kwa sababu Yohana Mbatizaji alizaliwa katika dunia hii, na wakati alipombatiza Yesu Kristo, dhambi za ulimwengu zilipitishwa kwenda kwa Yesu. Hivyo, Yesu aliweza kuzibeba dhambi za ulimwengu mara moja. Kwa kuruhusu jambo kuwa hivyo, Bwana amewaruhusu wale wanaoamini katika huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu kuingia Mbinguni kwa kupokea utakaso wa dhambi. Hii ndiyo maana iliyomo katika kifungu cha maandiko toka katika Injili ya Mathayo sura ya 11, aya ya 12-14. Je, unaamini kuwa injili ya maji na Roho ndiyo Ukweli? Ikiwa unaamini hivyo, basi hii ina maanisha kuwa unaifahamu huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu kikamilifu. Hata hivyo, Wakristo wengi ambao hawaifahamu huduma ya Yohana Mbatizaji hawaufahamu ukweli wa injili ya maji na Roho, na kwa sababu hiyo wanaishi maisha yao ya kiimani kwa jinsi ya matamanio ya miili yao. Pamoja na kuwa hawana ufahamu, watu wa jinsi hiyo hawajaribu hata kuifahamu huduma ya Yohana Mbatizaji iliyoandikwa katika Injili Nne. Kwa sababu hiyo, huduma ya Yohana Mbatizaji imekuwa haiheshimiwi kwa muda mrefu hata miongoni mwa Wakristo wanaodai kumwamini Yesu. Pengine kwa sababu hii, ninaona kuna watu wengi siku hizi ambao hawavutiwi na huduma ya Yohana Mbatizaji. Hivyo, watu wanakawaida ya kuwashangaa wale wanaovutiwa na mada hii. Hii ni kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiitazama kwa mbali huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu kiubishi kwa muda mrefu.
https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35